1 Kings 9:23-27

23Pia walikuwa maafisa wakuu wasimamizi wa miradi ya Sulemani: maafisa 550 waliwasimamia watu waliofanya kazi.

24Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Sulemani alikuwa amemjengea, akajenga Milo.

25Sulemani akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejengea kwa ajili ya Bwana, akifukiza uvumba mbele za Bwana pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za hekalu.

26Mfalme Sulemani pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu.
Yaani Bahari Nyekundu au Bahari ya Mafunjo.
27Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Sulemani.
Copyright information for SwhKC